Tuesday, November 11, 2008

Umaskini


Watu wamewahi kuandika sana wakizingatia kuona halisi au kupitia majarida mbalimbali, leo nami naandika hasa baada ya kuguswa na umaskini ambao nimeouna hapa California San Diego. Mji wa San Diego ni mzuri sana umekaa kitalii hivi japo utalii unachukua nafasi ya tatu baada ya shughuli za kijeshi na teknolojia ya kibaiolojia.


Pamoja na yote nimeona watu maskini akina Matonya wakiombaomba tena wanasema hawana mahali pa kulala. Anatembea na vilago mahali popote anaweza kulala pale usiku ukiingia.


Kwa msingi huo umaskini huu ni wa mali (material possession) na pia kipato (income), kama wangekuwa na mali ya urithi kama nyumba basi wangeomba na jioni kwenda kulala kwao. Hapa nimegundua kuwa nchi ni tajiri lakini watu wake ni maskini wale hasa wasio nacho.


Kwa upande mwingine serikali yao iko makini sana na suala la kodi hakuna mianya ya kukwepa kodi watu wake wanajivua kulipa kodi, hata grocery imeandikishwa kulipa kodi, kodi ni msingi wa maendeleo yao hii imesaidia kupata huduma bora za jumla kama barabara zuri na usafi wa jiji.


Pia umaskini huu umeleta matabaka, utaona watu weusi baadhi ndiyo wanaofanya kazi ngumu wakimwemo na raia wa Mexico. Ndiyo wahudumu mahotelini naamini wanalipwa kiasi kidogo sana ambacho ni kama kamba waliyofungwa nayo hakuna kuikata, yaani mduara wa umaskini. Hivyo umaskini huzalisha umaskini, poverty breeds poverty, kweli tembea uyaone.


Karibuni kwa maoni yenu.

No comments:

Blog Archive

Powered By Blogger